"Elimika, Elimisha, Burudisha"

Vigezo na Masharti ya Jukwaa la Elimika

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili.

Mambo unayopaswa kuzingatia;

  • Kuhakikisha ujumbe wako una dhima kuu ya kuelimisha jamii au kuipasha jamii habari
  • Ujumbe wako uwe wa kweli na wenye kuzingatia maadili na tamaduni zetu (ni muhimu kuzingatia sheria ya mtandao)
  • Ikitokea umevunja sheria za kimtandao jukwaa letu halitahusika kwa lolote.
  • Hakikisha taarifa zako za siri unazifanya kuwa siri (Nywila yako hutakiwi kumuonesha mtu mwingine)
  • Toa taarifa mapema kupitia fomu ya mapendekezo pindi unaposhuku kuna kitu kinafanyika kwenye ukurasa wako kinyume na matakwa yako
  • Hakikisha unatumia jina lako sahihi, picha na eneo sahihi ulipo (Hii itakusaidia upate badge ya uthibitisho inayoonesha kuwa wewe ni mtumiaji halali wa jukwaa hili la elimu na Kiswahili.
  • Hakikisha unajiandikisha kwa ukurasa mmoja na maalum (Muhimu kuepuka kutumia kurasa vivuli)
  • Kutokana na mgawanyiko wa jukwaa letu, weka ujumbe wako kwenye sehemu husika ya jukwaa bila kuchanganya ili kuwasaidia watu kujadili mada zako kwa urahisi.
  • Ujumbe wako utatumika kutoa elimu kwa wengine kwa kusambazwa sehemu mbalimbali.

Muundo wa Jukwaa la Elimika

Jukwaa hili limegawanyika katika sehemu mbalimbali ili kukuwezesha kuuweka ujumbe wako kule unapolenga. Lugha inayozungumzwa ni Kiswahili pekee ili kumuwezesha hadi mtu ambaye hafahamu kwa undani lugha ngeni kuelewa kwa undani dhima ya ujumbe wako. Lengo letu ni kuufikia ulimwengu kwa lugha yetu zawa-Kiswahili.

Je, ninastahili kuwa mwanachama?

Lengo letu ni kuwafikia wengi na kuhakikisha jamvi hili kuwa sehemu ya mabadilishano ya uelewa stahiki wa mambo mbalimbali. Kama una umri kuanzia miaka 15, basi jukwaa hili linakufaa na kuwa huru kulitumia.

Muda gani niwe hewani?

Jukwaa hili liko hewani Saa 24, unaweza kuandika ujumbe wako wakati wowote na kuwa huru kutoa mawazo yako na kuwa tayari kutoa elimu kwa wengine ili wajifunze. Kwetu tunaamini kila mmoja ana kitu kipya cha kujifunza kutoka kwa mwengine na kipya kwake kujifunza toka kwa wengine.

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search