"Elimika, Elimisha, Burudisha"

 1. Yose Hoza
 2. Mchanganyiko
 3. Jumanne, 30 Januari 2018
USIMDHARAU USIYEMJUA.

Siku moja jioni Rais Obama alimshauri mkewe wakale dinner mtaani huko Washington ktk mgahawa wowote wa watu wa kawaida. Wakakubaliana kisha Obama akatoa taarifa kwa walinzi wake wawe tayari maana siku hiyo wataenda kupata chakula kwenye mgahawa wa mtaani.

Rais Obama na mkewe Michelle wakajiandaa. Ilipofika jioni Obama na Michelle wakiwa chini ya uangalizi mkubwa wa makachero wa CIA na FBI, wakaingia mtaani na kujichanganya bila kujulikana. Wakaingia kwenye restaurant moja ya watu wa kawaida wakakaa na kuagiza chakula.

Kwa kuwa ilikua restaurant ya kawaida, haikua na wahudumu wengi.. walikuwepo wahudumu wawili kwa upande wa chakula na upande wa vinywaji alihudumia mmiliki wa restaurant mwenyewe.. Hakuona haja ya kuajiri mtu kwenye vinywaji kutokana na faida ndogo anayoipata.

Hivyo alienda mwenyewe meza ya kina Obama na kuwasikiliza order ya vinywaji. Kwa kuwa Obama na mkewe walikua wamevaa mavazi casual, jamaa hakuwatambua kwa haraka. Akasikiliza order zao na kuwaletea vinywaji.. Walipomaliza kula na kunywa, yule mhudumu akahisi yule mwanamke ni Michelle, lakini hakuwa na uhakika.."..mke wa Rais anawezaje kuja kula mahali pa kimaskini kama hapa??" Alijiuliza yule mmiliki wa ule mgahawa ambae jina lake aliitwa Andrea.

"Sidhani... itakuwa nimemfanisha tu." Alizidi kuwaza. Lakini baadae akajishauri "ngoja tu nimuulize, kama si yeye basi, kuuliza si dhambi." Akajipa ujasiri kisha akaenda kwenye meza ya kina Obama na kuuliza "Samahani wewe ndiye Michelle, au mmefanana?" Akauliza Andrea.

"Hakika ni mimi, naweza kukusaidia nini? Akajibu Michelle kwa kujiamini. Lile jibu likamfanya Andrea azidi kutetemeka, na ule mshtko ukawa mkubwa hadi akina Obama wakajua ameshtuka..!

Mara machozi yakambubujika... ndani ya dakika 5 alibubujikwa machozi bila kusema neno. Obama akadhani ni hofu ya kuwaona pale, hivyo akamwambia "relax big man..feel safe." (Usihofu bwana mkubwa, jisikie huru).

Kisha Andrea akamgeukia Michelle na kumwambia mheshimiwa mke wa Rais, mimi ni Andrea, tulisoma wote sekondari St.Peters. Ghafla kumbukumbu zikamjia Michelle, akasimama na kumkumbatia Andrea. Akampatia business card yake kisha wakaondoka.!

Wakiwa kwenye gari wakati wanarudi Michelle akamwambia Obama "Mpenzi najua siri ya machozi ya yule mwanaume. Naweza kukushirikisha?" "Your wish my love" (Kama upendavyo mpenzi). Akajibu Obama kwa shauku ya kujua.!

"Ni mwanaume wa kwanza kumpenda lakini hakuheshimu kbs hisia zangu. Hakuwahi japo kuniambia "Nakupenda pia" hata mara moja, kati ya mara zote nilizomwambia nampenda).

"Pole mpnz, kwa hiyo kama angekuoa, kwa sasa ungekua mmiliki wa ule mgahawa mzuri tulioenda kula? Aliuliza Obama baada ya kumpa pole mkewe.!

"Hapana, kama angenioa kwa sasa ningekua mke wa Rais). Alijibu Michelle kwa kujiamini. "You are very funny my dear. How then?" (Una utani sana mpenzi.. kivipi sasa?) Aliuliza Obama.

Michelle akajibu kwa umakini "Kwa sababu angekua Rais." How honey? (kivipi mpenzi?) Aliuliza tena Obama kwa shauku.

"Kwa sababu nilimuomba Mungu niolewe na Rais. Na tangu utoto wangu nilijua nitaolewa na Rais. Hivyo kama Mungu angenipa Andrea kuwa mume wangu naamini angemfanya kuwa Rais." Alijibu Michelle.

Obama akakumbua kuwa yeye hajawahi kuomba kuwa Rais, lakini kumbe mkewe aliwahi kuomba kuolewa na Rais. Aakamtazama mkewe na kumkumbatia kisha akamwambia "Nakupenda Michelle"

MORAL OF THE STORY.!!

Tunajifunza mambo makubwa matatu kupitia story hii:

1. Wanaokudharau leo, siku moja watakusalimia kwa heshima. Andrea alimpuuza Michelle,lakini kwa sasa anatamani kuwa hata mtumishi wake.

2. Pili, nyuma ya mafanikio yako kuna mtu/watu waliofanya wewe kua hapo. Usijisahau. Waheshimu, wapende, wathamini, wajali. Nyuma ya Urais wa Obama alikuwepo Michelle. Obama hakuwahi kuomba kuwa Rais, lakini Michelle aliomba kuolewa na Rais. Hii ina maana kuwa mwanaume yeyote ambaye angemuoa Michelle angekua Rais wa Marekani.

3. Tatu, Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo. Ukimuomba Mungu na ukaamini basi jiandae kupokea muujiza wako. Usikate tamaa.. keep moving towards your goals hata ukikumbana na vikwazo vya aina gani. Michelle alimuomba Mungu aolewe na Rais, na alisimama ktk imani yake hadi mwisho. Haijalishi alipitia majaribu kiasi gani, haijalishi aliachwa na wangapi.. Alichoamini ni kuwa siku moja ataitwa mke wa Rais.

Je wewe unaesoma ujumbe huu umemuomba nini Mungu juu ya mwenzi wako? umemuomba nini Mungu juu ya maisha yako? Umemuomba nini Mungu juu ya biashara yako, kazi yako etc?

Nakutia moyo kuwa hata kama upo kwenye hali ngumu kiasi gani, usikate tamaa. Mweleze Mungu hitaji lako, kisha simama ktk imani yako hadi mwisho na Mungu atakupa kwa kadri ya hitaji la moyo wako.
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.


Hakuna maoni yoyote kwa sasa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni yako!
Guest
Wasilisha Maoni Yako
Sakinisha faili au picha kwenye mjadala huu kwa kubonyeza kitufe cha sakinisha hapa chini. Inapokea gif,jpg,png,jpeg,zip,rar,pdf
• Insert • Futa Sakinisha faili (Lisizidi ukubwa wa: 2 MB
Weka Eneo Ulipo

Kuweka eneo ulilopo wakati wa kutoa maoni yako inawezesha wajumbe kujua mahali ulipo.

Latitude:
Longitude:

Jukwaa la Elimika

Mijadala

Afya
 1. Mijadala 6
 2. MIjadala midogo
Kiswahili
 1. Mijadala 20
 2. MIjadala midogo
Michezo
 1. 1 post
 2. MIjadala midogo
Teknolojia
 1. Mijadala 8
 2. MIjadala midogo
Mchanganyiko
 1. Mijadala 18
 2. MIjadala midogo

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search