"Elimika, Elimisha, Burudisha"

 1. Njawa
 2. Mchanganyiko
 3. Alhamisi, 25 Januari 2018
Uongozi unaanzia ndani ya familia zetu, mkubwa anawajibika kuwaongoza wadogo zake hali kadhalika wazazi/walezi kwa watoto wao. Kila wakati unapofanya ushawishi kwa mtu au kikundi cha watu wafanye suala fulani kuna kiashiria cha uongozi ndani yake.

Uongozi unaanza hata pale walipo wawili au zaidi, kwa mantiki sio lazima iwe kwenye taasisi, iwe kanisani nakadhalika. Lakini pia iwe kuna muingiliano/mawasiliano baina ya marafiki au watu walio karibu.

Kutimiza ‘wajibu’ wa uongozi ni muhimu kwa kiongozi kuzingatia yafuatayo:

Umuhimu wa uongozi kwa kiongozi uwe na manufaa kwa pande zote yaani anayeongoza na anayeongozwa. Inapaswa kiongozi apate muda wa kuelezea anaowaongoza manufaa ya kile anacho nuia kukitimiza. Hii itawasaidia wote kwa pamoja kuelewa nini hasa matokeo ya kinacho tarajiwa kutekelezwa matarajio yao.

Ni namna gani kiongozi anaweza kumudu ‘staili’ tofauti kwa weledi hasa kulingana na mazingira anayokabaliana nayo. Mathalani wakati wa hali ya dharula ni tofauti na hali isiyo ya dharula hii inaweza kuwa kipimo cha namna ambavyo uongozi unabadilika kadiri ya mazingira.

Kiongozi kimsingi atambue anahusika katika kuwatumikia/wahudumia anaowaongoza kuliko yeye awe anahudumiwa. Dhamana kubwa inawekwa kwa waliompa nafasi sio kinyume chake. Kwa maana kiongozi anabaki kuwa mtumishi wa waliompa dhamana, awepo pale anapohitajika sio kumtafuta kwa ‘tochi’. Muhimu sana awe mtu wa watu mwenye kujichanganya na jamii yenye matukio mbalimbali.

Nafasi ya kuwapa maarifa, mbinu, uelewa na kuwawezesha wengine wakati wao wa kuongoza na kuwajibika unapofika ukingoni wengine wachukue kijiti. Anayechukua nafasi hana budi kupata ushauri pale inapobidi katika masuala mbalimbali. Wanasema ya kale dhahabu hasa pale hiyo hazina inapotumika kwa manufaa bila kuingilia utaratibu uliopo au kuharibu.

Kiongozi anapaswa kutenda anayo ‘hubiri’. Ikiwa uongozi una hamasisha watu kufuata miiko/maadili ambayo yeye mwenyewe haitilii maanani na kuifuata utafika wakati watu watakosa kuheshimu na kufanya yale ambayo wanaona ni sahihi matokeo ni msuguano baina ya pande mbili.

Ndani ya jamii na maisha yetu ya kila siku uongozi una nafasi kubwa, unachukuliwa kama muarobaini wa kutatua majibu ya matatizo kwa wanao waongoza. Upande wa pili tutilie maanani kutimiza wajibu kwa mtu mmoja mmoja (binafsi), ni chachu ya mabadiliko ngazi ya familia na jamii kwa ujumla. Mathalani unatupa takataka usiku mtaani ikifika mchana unalalamika watu wanaotupa takataka unajionndoa kwenye kuwajibika unaonyeshea vidole na lawama wengine. Tuwahamize ‘tuwasumbue’ lakini tuwe vinara wa kutimiza wajibu.

@davenjawa
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.


Hakuna maoni yoyote kwa sasa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni yako!
Guest
Wasilisha Maoni Yako
Sakinisha faili au picha kwenye mjadala huu kwa kubonyeza kitufe cha sakinisha hapa chini. Inapokea gif,jpg,png,jpeg,zip,rar,pdf
• Insert • Futa Sakinisha faili (Lisizidi ukubwa wa: 2 MB
Weka Eneo Ulipo

Kuweka eneo ulilopo wakati wa kutoa maoni yako inawezesha wajumbe kujua mahali ulipo.

Latitude:
Longitude:

Jukwaa la Elimika

Mijadala

Afya
 1. Mijadala 6
 2. MIjadala midogo
Kiswahili
 1. Mijadala 20
 2. MIjadala midogo
Michezo
 1. 1 post
 2. MIjadala midogo
Teknolojia
 1. Mijadala 8
 2. MIjadala midogo
Mchanganyiko
 1. Mijadala 18
 2. MIjadala midogo

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search