"Elimika, Elimisha, Burudisha"

 1. Yose Hoza
 2. Afya
 3. Jumatatu, 29 Januari 2018
Tatizo la sonona

Ugonjwa Sonona
Nahau Sononeka

Sonona ni ugonjwa wa kufadhaisha kwa muda mrefu amino humuathiri mtu na kumzuia kufanya kwa weledi shughuli zake za kila Siku

Hisia nyingi huwa za huzuni na kumfanya mtu ajihisi hafai mwenye hatia muda mwingi na kukosa amani kupwata na hofu ghafla na kushindwa kufanya mambo kwa ufasaha

Sonona humfanya mtu kuwa na huzuni mnyonge dhaifu na kujihisi ametengwa

Jinsi ya kujitambua Kama una Sonona

1.HUZUNI
Muda mwingi unakuwa mtu mwenye huzuni na kujihisi huna thamani hufai huna tumaini

Kwa kawaida binadamu unaweza kuwa na huzuni kama vile ukipata Msiba kuugua kuuguliwa lakini huzuni ya sonona mara nyingi hukupata kwa majuto

2.KUJITENGA
Hali hii humkuta mtu mara nyingi kutokupenda kushiriki shughuli za pamoja Kama vile ndani ya familia mtoto kukaa peke yake muda mrefu na kuwa na mawazo pasi furaha

3.HAMU YA CHAKULA
Mtu mwenye sonona hukumbwa na hali ya kutokuhisi hamu ya kula moyoni kama vile anahukumiwa

Mtu mwenye sonona huweza kuwa hali kabisa au kula kwa kupita kiasi
Hii hupelekea kukonda au kunenepa kupita kiasi

4.MABADILIKO YA HALI YA USINGIZI
Usingizi wa mtu mwenye sonona waweza kuwa analala sana au anakosa kabisa usingizi

Mtu mwenye Sonona anaweza kuwa anaamka usiku na Hali tena mpaka kunakucha muda wote anakuwa na mawazo ya kumuumiza kumfedhehesha na kufikiri hata kufa

Kukosa usingizi husababisha kinga ya Mwili kushuka na magonjwa nyemelezi kuushambulia Mwili

5.UCHOVU ULIO PITILIZA
Mtu mwenye sonona huwa na uchovu uliopitiliza bila kuwa amefanya kazi nzito

Akili huwa imechoka na msongo wa mawazo yasiyo na majibu mepesi na huhitaji muda mrefu wa kupumzika ili kutua mzigo mzito

Uchovu husababisha ufanisi wa kufanya kazi kupungua na kumbukumbu kujirudi mfadhaiko huweza mfanya mtu akalia peke yake wengine huzimia na kuanguka baada ya hisia Kali kuushambulia moyo

6.KUJIHISI
Mtu mwenye sonona hujihisi muda wote ana hatia mara
Mara nyingi hutafsiri mambo katika hasi

7.KUJIUA
Msongo wa mawazo unapo shambulia sana moyo huleta mfadhaiko kujutia kujiona huna thamani kutafsiri dunia hasi na kukosa tumaini

Sonana husababisha sana kujiona una hatia na kuwaza kuhusu kifo muda mwingi

Wanawake wenye SONONA hujaribu kujiua zaidi ya Wanaume. Lakini wanaume hufanikiwa zaidi KUSUDIO la KUJIUA

Wanawake hutumia njia laini kujiua Kama kunywa vidonge, sumu Wanaume hutumia njia Tata kama Kujinyonga kujipiga Risasi

Kwa wanaume walio Single na kuishi peke yake muda mrefu huwa na hatari kubwa ya kijiua

VIHATARISHI VINAVYOWEZA KUKUPATIA SONONA

1.URITHI WA KIFAMILIA
Watu wenye ndugu wa karibu (Ndugu wa damu)
Wana hatari Mara 2 au 4 zaidi ya kupata Sonona hurithi kwa njia ya Kibaolojia

2.MIKAZO YA KIMAISHA
Sonona huwapata watu wenye daraja la chini la kiuchumi kutokana na changamoto wakutanazo kwenye maisha hali ngumu (Ugumu wa kimaisha)

3.HISIA HASI
Watu ambao wanaona hasi katika kila jambo walifanyalo hushambuliwa sana na SONONA na kupata msongo hatari wa mawazo (STRESS)

4.MAZINGIRA
Mfano: Mtu aliyetendwa vibaya Utotoni hata Ukubwani kama vile KUBAKWA hushambuliwa na SONONA muda mrefu wa maisha yao na kukosa amani

Mifano mingine Kuteswa, Kutekwa kushuhudia familia ikuungua na moto na wewe ndiye uliye bahatika kupona, Ajali mbaya

5.MAGONJWA YA KUDUMU
Kisukari, magonjwa ya Moyo unene kupitiliza kupita kiasi

6. MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA
Madawa ya kulevya hushambulia Ubungo na moyo na humuacha mtumiaji katika ghazabu ya muda mrefu na kuathiri uwezo wa kufikiri kutenda kazi

JINSI YA KUTIBU SONONA
1.MAAMUZI
Unapokuwa na changamoto nyingi jitahidi kufanya maamuzi yanayo Leta faraja na mashauri yako yawe kwenye chanzo kinacho tegemeka

2.BADILI MTAZAMO
Fikra unazo zijenga jitahidi ziwe na mawazo chanya ni vyema kupata ushauri wa watu ili kujua mbinu zitumikazo uwe na matumaini utafanikisha

Waweza tafuta dakrari wa masuala ya kiakili wengi wanao ugua magonjwa ya akili huogopa kutafuta matibabu kutokana na kuwaza Jamii itakavyo wachukulia

Mawasiliano mazuri Kati ya mgonjwa na daktari lazima yawepo

3.TUNZA AFYA YA MWILI NA AKILI
Lishe bora Fanya mazoezi ya kutosha pumzika soma vitabu piga story Na watu tofauti tofauti badili mazingira inapobidi

Mazoezi huzalisha kemikali inayo kufanya ujihisi vizuri, kukuchangamsha, na kukufanya ujihisi vizuri

4.BADILI MFUMO WA MAISHA
Kuacha mambo yanayo pelekea kujuta kunung'unika kukataa tamaa kukupa huzini maana mfumo wa maisha una uhusiano mkubwa na Ubongo na mwili

Kumbuka
Nafasi uliyonayo ya kupumua hukupa sababu bilioni ya kuwa na furaha Epuka SONONA
Attachments (5)
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.


Hakuna maoni yoyote kwa sasa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni yako!
Guest
Wasilisha Maoni Yako
Sakinisha faili au picha kwenye mjadala huu kwa kubonyeza kitufe cha sakinisha hapa chini. Inapokea gif,jpg,png,jpeg,zip,rar,pdf
• Insert • Futa Sakinisha faili (Lisizidi ukubwa wa: 2 MB
Weka Eneo Ulipo

Kuweka eneo ulilopo wakati wa kutoa maoni yako inawezesha wajumbe kujua mahali ulipo.

Latitude:
Longitude:

Jukwaa la Elimika

Mijadala

Afya
 1. Mijadala 6
 2. MIjadala midogo
Kiswahili
 1. Mijadala 20
 2. MIjadala midogo
Michezo
 1. 1 post
 2. MIjadala midogo
Teknolojia
 1. Mijadala 8
 2. MIjadala midogo
Mchanganyiko
 1. Mijadala 18
 2. MIjadala midogo

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search