"Elimika, Elimisha, Burudisha"

 1. Yose Hoza
 2. Mchanganyiko
 3. Jumamosi, 20 Januari 2018
ONGEZEKO LA THAMANI YA SHILINGI YETU

Thamani kubwa/ndogo ya SHILINGI inajalisha hali ya mustakabali wa biashara, deni la Taifa, vipato, uwekezaji uzalishaji wa bidhaa

Katika soko ambalo serikali huingilia nguvu ya SOKO kwa mkono wake usioonekana, Thamani hii haitegemei nguvu ya SOKO bali maamuzi mbalimbali yakiwemo ya KISIASA kwa kiasi kikubwa

Tanzania ilikuwa katika hali hii Kati ya mwaka 1967 hadi mageuzi makubwa ya kiuchumi miaka ya 1980

Mambo yanayo changia ONGEZEKO la shilingi yetu

1.Mauzo ya bidhaaa na huduma
2.Manunuzi ya bidhaa toka Nje
3.Misaada Na Uwekezaji
4.Wafanyakazi nje ya nchi

1.Mauzo ya bidhaa na huduma

Malighafi inayozalishwa nchini ikiweza jitosheleza na kuuzwa nje ya nchi Taifa huingiza sarafu yetu katika masoko makubwa ya kibiashara na huingizwa katika mabadilishano ya fedha na mataifa makubwa

Kadri malighafi inapopanda thamani ndivyo na shilingi yetu inavyokua kwa kasi

Kunapokuwa na fedha nyingi za kigeni Kama vile Dola katika uchumi, bei yake katika kiwango cha kubadili fedha hushuka, Bei ya Dola inaposhusha SHILINGI yetu ina imarika

Sekta kama ya UTALII hutuingizia fedha nyingi za kigeni kutokana na Thamani ya Mbuga zetu kuwa na aina mbalimbali za wanyama wanaovutia watalii

Thamani ya fedha ya mauzo ya nje inapokuwa kubwa kuliko MANUNUZI kutoka nje ya NCHI Kuna uwezekano wa Thamani wa SHILINGI Yetu kuongezeka

Bidhaa zinapokuwa bora zaidi GRADE A huleta ushindani mkubwa katika soko la nje

Uuzaji wa madini Kama Tanzanite huchangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha SHILINGI yetu bidhaa adimu inayopatikana Tanzania pekee

Usindikaji wa mazao maziwa ngozi za wanyama magogo mbao n.k huchangia kuimarisha SHILINGI

"UHALISIA" Ni kwamba mauzo ya nje ya Tanzania huleta fedha kidogo kuliko zinazotoka NCHINI kwenda NJE katika miamala ya kimataifa kulipia manunuzi kutoka NJE

2. MANUNUZI KUTOKA NJE

Tanzania haiwezi kuishi Kama KISIWA bila kutegemea bidhaa au huduma kutoka nje ya nchi

Hakuna nchi inayojaaliwa rasilimali zote zinazo hitajika kuzalisha bidhaa na huduma zinazo kidhi NCHI husika

Ni muhimu kwa nchi kupunguza manunuzi ya bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi Kama njia mojawapo kuepuka KUSHUKA Kwa Thamani ya SHILINGI ~~> "Hata hivyo ni Lazima kuwepo kwa Bidhaa na Huduma bora zinazo zalishwa NCHINI kwa Wingi" ili walaji na watumiaji watende haki katika Manunuzi

4.MISAADA NA UWEKEZAJI

Tanzania hupokea misaada toka nchi mbalimbali misaada hii huwa fedha za kigeni Kama vile Dola japokuwa hatupaswi kutegemea misaada.

Misaada huja kwa sura ya fedha za kigeni na kusaidia KUIMARISHA shilingi yetu

UWEKEZAJI

Wawekezaji wakubwa wanakuja nchini huchangia kuimarisha shilingi kwa kiasi kikubwa cha fedha za kigeni wanapo tengeneza miradi

Wawekezaji huzalisha bidhaa na huduma bora kwa wingi na kuingiza katika soko la ushindani kufanya Shilingi yetu izidi kupaa

4.Watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi

Fedha za kigeni wanazotuma Nchini Dola huingia katika mfumo wa kibenki na kubadilishwa kuwa SHILINGI
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.


Hakuna maoni yoyote kwa sasa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni yako!
Guest
Wasilisha Maoni Yako
Sakinisha faili au picha kwenye mjadala huu kwa kubonyeza kitufe cha sakinisha hapa chini. Inapokea gif,jpg,png,jpeg,zip,rar,pdf
• Insert • Futa Sakinisha faili (Lisizidi ukubwa wa: 2 MB
Weka Eneo Ulipo

Kuweka eneo ulilopo wakati wa kutoa maoni yako inawezesha wajumbe kujua mahali ulipo.

Latitude:
Longitude:

Jukwaa la Elimika

Mijadala

Afya
 1. Mijadala 6
 2. MIjadala midogo
Kiswahili
 1. Mijadala 20
 2. MIjadala midogo
Michezo
 1. 1 post
 2. MIjadala midogo
Teknolojia
 1. Mijadala 8
 2. MIjadala midogo
Mchanganyiko
 1. Mijadala 18
 2. MIjadala midogo

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search