"Elimika, Elimisha, Burudisha"

 1. Julius Kiting'ati
 2. Mchanganyiko
 3. Jumamosi, 20 Januari 2018
Biashara ya anga inavutia sana ,
hasa kutokana na teknolojia kushika kasi huku kila shirika likijaribu kuwapatia wateja wake huduma bora wakiwa wanatoka sehemu moja kuelekea sehemu nyingine. Hii inadhihirika baada ya ushindani mkuea kati ya kampuni ya kutengeneza body ya Boeing ( Marekani ) na Airbus ( Ufaransa ). Airbus A-380 ni ndege kubwa sana duniani kwa sasa , yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 800 na pia kutembea umbali wa zaidi ya 15,000 Km yaani kuifanya kutoka Marekani mpaka Singapore bila kusimama kokote. Hii ni ndege imetengenezwa na kampuni ya Airbus ambayo ina makao makuu yake katika mji wa Teleousse Ufaransa. Ilitengenezwa ili kuendana na ushindani wa ndege za kupakia abiria duniani , kwa muda huo Boeing kampuni ya marekani ndio ilikuwa inashikilia rekodi ya kuwa na ndege kubwa ya Abiria duniani.

Airbus A -380 kwa mara ya kwanza iliruka kwa majaribio katika mji wa Telousse Ufaransa , ilikuwa 27/4/2005 lakini baada ya kujiridhisha na matumizi yake kampuni ya Singapore Airlines ilinunua ndege ya kwanza na kuanza safari zake mnamo 25/10/2007.Ni dhahiri kwamba Airbus inahitaji uwanja mkubwa sana na vifaa vya kisasa kuweza kuipokea na kuirusha angani ikiwa salama , hivyo kufanya itue katika viwanja vichache sana duniani. Kwa hapa Afrika inatua katika uwanja wa Bole ulioko Ethiopia , OR- Tambo ulioko Afrika kusini na Nigeria katika jiji la Lagos.

kwa sasa duniani ni mashirika 13 ya ndege ambayo yanatumia Airbus A -380 katika safari zake sehemu mbalimbali , huku waarabu wa dubai Emirates wakiongoza kwa kuwa na ndege hizo kubwa zaidi ya 130 katika safari zake.

 • Singapore Airlines
 • Emirates
  Qantas
  Airfrance
  Lufthansa
  Korean Air
  China southern Airlines
  Malysian Airlines
  Thai Airways
  British Airways
  Asian Airlines
  Qatar Airways
  Etihad Airways


uchambuzi wa ndege hiyo kwa vipimo mubashara.

1.Urefu wa mita 72.7 yaani nusu na robo ya uwanja wa kisasa wa mpira.

2.Upana wa mita 79.7 kutoka kwenye ncha ya bawa moja mpaka ncha ya bawa nyingine.

3.Kimo cha mita 24.

4.Uzito wa tani 577.

5.Inatembea umbali wa kufikia Kilometa 15,000.

6.Inabeba mafuta ya ujazo wa Lita 323,545.


kwa ukubwa wa ndege hiyo na teknolojia yake , abiria wa kutoka Tanzania hawajaonja huduma zake.
Attachments (13)
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.
Yose Hoza Accepted Answer Pending Moderation
0
Kura
Undo
Watu 800 ka mji hivi
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.
 1. zaidi ya mwezi 1 uliopita
 2. Mchanganyiko
 3. # 1
AbbyMexahnk Accepted Answer Pending Moderation
0
Kura
Undo
Aisee... Si Mchezo
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.
 1. zaidi ya mwezi 1 uliopita
 2. Mchanganyiko
 3. # 2
 • Kurasa :
 • 1


Hakuna maoni yoyote kwa sasa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni yako!
Guest
Wasilisha Maoni Yako
Sakinisha faili au picha kwenye mjadala huu kwa kubonyeza kitufe cha sakinisha hapa chini. Inapokea gif,jpg,png,jpeg,zip,rar,pdf
• Insert • Futa Sakinisha faili (Lisizidi ukubwa wa: 2 MB
Weka Eneo Ulipo

Kuweka eneo ulilopo wakati wa kutoa maoni yako inawezesha wajumbe kujua mahali ulipo.

Latitude:
Longitude:

Jukwaa la Elimika

Mijadala

Afya
 1. Mijadala 6
 2. MIjadala midogo
Kiswahili
 1. Mijadala 20
 2. MIjadala midogo
Michezo
 1. 1 post
 2. MIjadala midogo
Teknolojia
 1. Mijadala 8
 2. MIjadala midogo
Mchanganyiko
 1. Mijadala 18
 2. MIjadala midogo

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search