"Elimika, Elimisha, Burudisha"

 1. Julius Kiting'ati
 2. Mchanganyiko
 3. Jumatano, 07 Machi 2018
Kuna siku moja nilikuwa natembea na kukutana na mtu mmoja wa makamo wa umri na alikuwa anaongea na simu , kwa maongezi yale alikuwa anatoa ushauri kwa mtoto wake wa kiume ambaye alikuwa anasoma katika chuo kikuu. Nilisikia akisema , “ mwanangu , mwanamke ndio nguzo ya maendeleo yako. Omba kwa mungu akuongoze kwa hilo “. Maneno haya yalinigusa mimi , na ulimwengu umekuwa mahali Salama kwa kuishi maneno hayo ya hekima.
Mwanamke katika historia ya dini alikuwa ni ubavu wa kiume na lengo kuu ilikuwa kusaidia katika kazi ya kuitunza dunia. Kuanzia zama zile za zamani , alikuwa na kazi ya kusaidia. Lakini kutokana na mabadiliko makubwa sana katika zama hizi , mwanamke anakuwa na nafasi kubwa sana ya kufanya mabadiliko na kuwa nguzo kwa jamii bora. Analea , anatunza na anabadilisha muonekano wa jamii. Nina imani kila mmoja wetu anakuwa na faraja sana akiwa katika mikono ya mama yake.
Fursa kwa mwanamke katika jamii ya sasa ni pana sana , kutoka katika uvumbuzi wa teknolojia mpaka kuwa kiongozi bora kwa jamii. Unamkumbuka Maria Thatcher ? alikuwa ni waziri mkuu wa kwanza mwanamke uingereza , alichpa kazi na kuitwa jina la utani , “ IRON LADY “ yaani mwanamke wa chuma. Alikuwa ni kinara katika kazi yake na aliaminisha wananwake wa ulaya kwamba wanaweza kuwa viongozi wa mataifa makubwa. Tukirudi katika bara letu pendwa la Afrika , mwanamke wa kwanza kutunukiwa tuzo ya nobel ya mazingira ni Wangari Mathai , kutoka Kenya nchi jirani tu hapo. Hakika nguzo ya jamii na maendeleo ni mwanamke!
Nina imani kubwa sana kwamba kutakuwa na ushirikishwaji kwa mwanamke katika jamii, taasisi ya umoja wa mataifa ikiwa kama taasisi mama katika kupigania haki za mwanamke duniani inakuwa katika nafasi nzuri kuwa na mipango mikakati bora ili kuhakikisha haki ya mwanamke inapatikana. Tanzania ni katika nchi za afrika ambazo hufanya vizuri sana katika kupigania haki za mwanamke na kumpatia nafasi katika kila lifanyikalo aidha katika jamii , uongozi na pia ugunduzi. Nazidi kutoa kongole kwa mwanamke wa kitanzania ambaye kila kukicha anahangaika kugundua kitu kwa taiafaletu hili , tunajivunia sana amani na ustwawi wa jamii.
Unaweza kutiririka na majina ya wanawake wanaotoa hamasa kwa dunia kufanya mambo bora kila siku , napongeza sana juhudi zao….
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.


Hakuna maoni yoyote kwa sasa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni yako!
Guest
Wasilisha Maoni Yako
Sakinisha faili au picha kwenye mjadala huu kwa kubonyeza kitufe cha sakinisha hapa chini. Inapokea gif,jpg,png,jpeg,zip,rar,pdf
• Insert • Futa Sakinisha faili (Lisizidi ukubwa wa: 2 MB
Weka Eneo Ulipo

Kuweka eneo ulilopo wakati wa kutoa maoni yako inawezesha wajumbe kujua mahali ulipo.

Latitude:
Longitude:

Jukwaa la Elimika

Mijadala

Afya
 1. Mijadala 6
 2. MIjadala midogo
Kiswahili
 1. Mijadala 20
 2. MIjadala midogo
Michezo
 1. Mijadala 2
 2. MIjadala midogo
Teknolojia
 1. Mijadala 8
 2. MIjadala midogo
Mchanganyiko
 1. Mijadala 19
 2. MIjadala midogo

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search