"Elimika, Elimisha, Burudisha"

 1. Njawa
 2. Kiswahili
 3. Jumapili, 21 Januari 2018
Riwaya ya Wasifu wa Siti Binti Saad iliyo andikwa na Hayati Sheikh Shaaban Robert ni Kati ya kazi bora za Fasihi Andishi.

Hii ni Riwaya ya kihistoria ambayo inasumulia kuhusu maisha ya Siti Binti Saad kisiwani Unguja. Maisha ya Siti yanaelezwa tangu utotoni kutoka familia duni. Lakini juhudi zake mwenyewe Siti anafanikiwa 'kutoboa' na kufanikiwa katika maisha kwa kuzalisha mali na uimbaji taarabu. Shughuli ambayo iliinua kipato chake na kuweza kumpa sifa zilizo enea Unguja, Afrika Mashariki na nje ya bara la Afrika. Siti Binti Saad alifanya shughuli za uimbaji hadi mauti yalipo mfikia Juni 1950.

Shabaan Robert amejadili ukombozi wa kifikra, kiutamaduni na kiuchumi. Mfano mhusika mkuu Siti Binti Saad kuonyesha njia halali za kujikomboa kiuchumi kwa Kutumia juhudi zetu na vipawa tulivyonavyo ili kuinua vipato vyetu.

Ukombozi wa kiuchumi, ni zao la kazi. Kazi yoyote ya halali ni kipimo cha utu, heshima na kuwajibika. Siti alizaliwa katika familia maskini baadaye anajishughulisha na ufinyanzi, anafanya biashara ya uchuuzi na hatimaye anaingia kuimba taarabu ulimpa kipato na kumuinua.

Riwaya hii inawasilisha dhamira zifuatazo. Umuhimu wa Elimu, Namna ya kuishi na watu, Maadili mema na Ujasiri na uvumilivu katika maisha.
Kwa kuangalia dhamira chache ambazo zina akisi wakati wa maisha uliopo.

Ujasiri na uvumilivu ni suala muhimu Sana, Siti amevumilia kero mbalimbali kutoka kwa watu wanao mzunguka. Uvumilivu wake una changia kupiga hatua. Mathalani waimbaji walipo mtungia wimbo wa kumsengenya baada ya kuona anafanikiwa lakini aliweza kuvumilia.

Elimu na Jamii, Shaaban Robert anatumia Riwaya hii kufukishia ujumbe hata kwa kizazi cha wakati uliopo.

Maisha ni mapambano ili tuweze kuyamudu ni hazina tufanye kazi kwa bidii, tuwe na ujasiri pamoja na uvumilivu.

Uvumilivu na Ujasiri, umoja na mshikamano, elimu pamoja na kufanya kazi kwa bidii ni njia ya ukombozi.

Kazi ni msingi wa maisha.

Mfumo wa makazi bora ndio utukao tuwezesha kujikomboa katika jamii.

Kwa ujumla mwandishi anaeleza kwamba maisha ya binadamu ni mfululizo wa mapambano yenye lengo maalumu.

Tukipata muda tujenge ada ya kusoma vitabu sio lazima viwe riwaya, tamthilia au ushairi. Ikiwa ni mjasiriamali, mhasibu, mwalimu nakadhalika vinasaidia kuongeza maarifa na ufahamu katika maisha yetu ya kila siku kulingana na taaluma au shughuli unayo fanya.
  Dar es Salaam, Tanzania
Visit 
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.


Hakuna maoni yoyote kwa sasa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni yako!
Guest
Wasilisha Maoni Yako
Sakinisha faili au picha kwenye mjadala huu kwa kubonyeza kitufe cha sakinisha hapa chini. Inapokea gif,jpg,png,jpeg,zip,rar,pdf
• Insert • Futa Sakinisha faili (Lisizidi ukubwa wa: 2 MB
Weka Eneo Ulipo

Kuweka eneo ulilopo wakati wa kutoa maoni yako inawezesha wajumbe kujua mahali ulipo.

Latitude:
Longitude:

Jukwaa la Elimika

Mijadala

Afya
 1. Mijadala 6
 2. MIjadala midogo
Kiswahili
 1. Mijadala 20
 2. MIjadala midogo
Michezo
 1. 1 post
 2. MIjadala midogo
Teknolojia
 1. Mijadala 8
 2. MIjadala midogo
Mchanganyiko
 1. Mijadala 18
 2. MIjadala midogo

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search