"Elimika, Elimisha, Burudisha"

 1. Paschal Masalu
 2. Mchanganyiko
 3. Ijumaa, 19 Januari 2018
Habari Tanzania na Ulimwengu mzima!

Naitwa Paschal Masalu, Mwanzilishi wa Jukwaa hili la Elimu.
Awali ya yote nikushukuru kwa kuingia kwenye Tovuti hii maalumu kwaajili ya Elimu na kukubali kusoma mjadala huu. Ninaandika maneno haya huku nikiwa na furaha nyingi kwani safari ya ndoto yangu ya kuitumikia jamii imeanza vyema.

Kwa muda mrefu nimekua muathirika wa mitandao ya kijamii, nimepoteza muda mwingi kwa kufanya mambo yasiyo na tija kwa jamii yangu. Mwaka 2015 nikiwa bado masomoni nilipata wazo la kuisaidia jamii ambayo inahitaji elimu ya msingi na hawawezi kuipata. Nilikosa pa kushika, nilijiuliza naanzia wapi? Nikakumbuka jamii hii ninayoifikiria ndo jamii ambayo nipo nayo mtandaoni. Ndipo taratibu wazo la #ElimikaWikiendi kupitia Twitter lilipoanza kujijenga.

Nimejifunza mambo mengi sana, kwani mimi si mtu maarufu na sikuwa na nguvu yoyote ya kuivuta jamii ila kwa wazo la kuipa elimu. Japo mwanzo ulikuwa mgumu, lakini nilifurahishwa sana na upendo mwingi wa wadau wa elimu bila kujali udogo wa taaluma yangu, umri wala jina, ila walipokea nilichokuwa nacho. Nimejifunza kuwa nia ni jawabu.

Kuna wakati ilifika nilitaka kuacha kabisa jambo hili, lakini nilipata nguvu kubwa kutoka kwa Mlezi wangu (Ndugu Kiiya JK), wadau wangu wa jamvi la elimika, na ndugu na jamaa. Hii ilinipa nguvu sana, nikafahamu kuwa kuna muda jambo lako ukishaliweka kuwa la jamii, jamii itakusaidia kulibeba.

Nia yangu hasa iliyokuwa inapiga kelele ni kuwa na Tovuti maalumu ambayo itakuwa jukwaa la wadau wa elimu, waje kujifunza na kuwafundisha wengine kwani upo usemi usemao, "Kila unaekutana nae ana jambo la kukufunza." Leo hii tuna Jukwaa hili la Elimika, ninajua jamii italifahamu vyema na kitakuwa chombo muhimu kwa nchi yetu Tanzania na ulimwengu mzima.

Rai yangu kwa vijana:
1. Usife moyo kwa kitu unachokipenda
2. Hakikisha una mshauri (mlezi)
3. Heshimu kila mtu unaekutana nae hata kama humfahamu kabisa
4. Usivunjwe moyo na mwitikio hafifu wa jambo lako, maneno yajayo kinyume na kila aina ya ukinzani

Kumbuka: Huwezi kupendwa na kila mtu, lakini jua kuna mtu unaokoa maisha yake kwa kazi yako ndogo unayoifanya.

Nikushukuru tena, kwa kutoa muda wako na kuwa sehemu ya Jukwaa hili la elimu. Leo tupo wachache, lakini kesho yetu ina wadau wengi. Nitausoma tena ujumbe huu baada ya miaka mitano ijayo. ASANTE!

Rejea:
Kuhusu #ElimikaWikiendi (Habari na The Citizen)

Makala maalumu toka Gazeti la Mwananchi, kuhusu #ElimikaWikiendi

Makala maalumu toka Raleigh International nchini Uingereza, Kuhusu #ElimikaWikiendi
Attachments (1)
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.
Ida Mwingira Accepted Answer Pending Moderation
0
Kura
Undo
Tupo pamoja, nakuombea uzima na afya pamoja na familia nzima ya ElimikaWikiendi. Nina Imani itakuwa faraja kubwa ukija kusoma ujumbe huu baada ya miaka mitano.
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.
 1. wiki 4 zilizopita
 2. Mchanganyiko
 3. # 1
Yose Hoza Accepted Answer Pending Moderation
0
Kura
Undo
Makala hizo hujaweka Link ndugu
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.
 1. wiki 3 zilizopita
 2. Mchanganyiko
 3. # 2
daudi Accepted Answer Pending Moderation
0
Kura
Undo
Inatia moyo
  Arusha, Tanzania
Visit 
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.
 1. wiki 3 zilizopita
 2. Mchanganyiko
 3. # 3
 • Kurasa :
 • 1


Hakuna maoni yoyote kwa sasa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni yako!
Guest
Wasilisha Maoni Yako
Sakinisha faili au picha kwenye mjadala huu kwa kubonyeza kitufe cha sakinisha hapa chini. Inapokea gif,jpg,png,jpeg,zip,rar,pdf
• Insert • Futa Sakinisha faili (Lisizidi ukubwa wa: 2 MB
Weka Eneo Ulipo

Kuweka eneo ulilopo wakati wa kutoa maoni yako inawezesha wajumbe kujua mahali ulipo.

Latitude:
Longitude:

Jukwaa la Elimika

Mijadala

Afya
 1. Mijadala 6
 2. MIjadala midogo
Kiswahili
 1. Mijadala 20
 2. MIjadala midogo
Michezo
 1. 1 post
 2. MIjadala midogo
Teknolojia
 1. Mijadala 8
 2. MIjadala midogo
Mchanganyiko
 1. Mijadala 18
 2. MIjadala midogo

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search