"Elimika, Elimisha, Burudisha"

 1. Kiiya
 2. Kiswahili
 3. Ijumaa, 02 Februari 2018
Kenya nasikiya
Urais kajiapishiya
Yao demokrasiya
Si yetu Tanzaniya

Rwanda
Uganda
Kabinda
Ijenda
Museveni kaganda
Kagame kaganda
Kabila Kaganda
Kurunzinza kaganda

Ima ni ukomavu
Ima katiba chakavu
Katiba mpya ni nguvu?
Majirani wa Bukavu
Waenenda kwa mabavu
Katiba mpya si nguvu
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.
Baraka Accepted Answer Pending Moderation
0
Kura
Undo
SHAIRI : KENYA

Wanisonona mtima, moyo wangu wanihima.
Pate radhi za karima, taa karibu kuzima.
Yaendeleayo si mema, sina budi kuyasema.
Hakika! Mungu yu mwema, atawanusuru vyema.

Ni fedheha na aibu, kwa yanayo wasibu.
Halihitaji tabibu, jazba wala ghadhabu.
Na hatupaswi ububu, kwakweli haliajibu.
Hakika! wenu wajibu, mshikamano ghalibu.

Nchi mwaiharibu, kwa tamaa ya vyeo.
Mwajijaza maswaibu, kukhofu maendeleo.
Enyi wetu mashaibu, fikirini kwa upeo.
Hakika! wenu wajibu, ni umoja kila leo.

Hakuna mkamilifu, mwoneshao udhaifu.
Ukabila ni vunjifu, mfanyayo kinaifu.
Afrika yetu tiifu, tunzeni uadilifu.
Hakika! wenu wasifu, muutunze kamilifu.

Kama hakua wa haki, je na wa sasa yu haki!
Nani mwerevu abaki, shupavu si mamluki.
Na yupi mtamalaki, muweze kumbariki.
Hakika! wata dhihaki, madhilani mkibaki.

Chuki huzika busara, pia leta matabaka.
Wanawafanya kafara, nyie ndio wadhulika.
Basi vuteni taswira, damu itapomwagika.
Hakika! mtazurura, ukimbizi kiwafika.

Watang'ata wapulize, kinafiki jisogeze.
Mazuri wazungumze, mabaya wayapenyeze.
Enyi watu msikize, amaniyo muitunze.
Hakika! muwabanguze, kwa amani muitunze.

Tamati yangu moyoni, kalamu imkononi.
Yasibuyo majirani, yazunguka ubongoni.
Niombacho ni amani, ajalie Maanani.
Hakika! ninaimani, hamtabaki juani.

Baraka Jereko
2/2/2018
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.
 1. wiki 3 zilizopita
 2. Kiswahili
 3. # 1
 • Kurasa :
 • 1


Hakuna maoni yoyote kwa sasa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni yako!
Guest
Wasilisha Maoni Yako
Sakinisha faili au picha kwenye mjadala huu kwa kubonyeza kitufe cha sakinisha hapa chini. Inapokea gif,jpg,png,jpeg,zip,rar,pdf
• Insert • Futa Sakinisha faili (Lisizidi ukubwa wa: 2 MB
Weka Eneo Ulipo

Kuweka eneo ulilopo wakati wa kutoa maoni yako inawezesha wajumbe kujua mahali ulipo.

Latitude:
Longitude:

Jukwaa la Elimika

Mijadala

Afya
 1. Mijadala 6
 2. MIjadala midogo
Kiswahili
 1. Mijadala 20
 2. MIjadala midogo
Michezo
 1. 1 post
 2. MIjadala midogo
Teknolojia
 1. Mijadala 8
 2. MIjadala midogo
Mchanganyiko
 1. Mijadala 18
 2. MIjadala midogo

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search