"Elimika, Elimisha, Burudisha"

 1. Baraka
 2. Kiswahili
 3. Alhamisi, 08 Februari 2018
Hiki cha leo kizazi,
Ni cha pesa bila kazi,
Hiki cha leo kizazi,
Cha wazazi si walezi.

Hiki cha leo kizazi,
Ni majani si mizizi,
Hiki cha leo kizazi,
Wajuaji si wajuzi.

Kimejaliwa makuzi,
Na sauti za miluzi,
Sifa zao ziku hizi,
Mojawapo ni uzinzi.

Hiki cha leo kizazi,
Kimejawa na ajizi,
Mabaya kwao ni ngozi,
Wala mema hakiwazi.

Wao watamani njozi,
halisia gozigozi,
Wapenda utandawazi,
Ilihali si wawazi.

Hiki cha leo kizazi,
Kinataka kuwa ngizi,
Hiki cha leo kizazi,
Ukweli wao mnazi.

Hiki cha leo kizazi,
Hakioni yangu kazi,
Ushairi kwao ngazi,
Haki kupanda hakiwezi.

Basi mie niwe wazi,
Sie wa leo kizazi,
Ndio tuwaangamizi,
Na ndio tuwakombozi.

Baraka Jereko
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.
Yose Hoza Accepted Answer Pending Moderation
0
Kura
Undo
Dah kweli kabisa
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.
 1. wiki 2 zilizopita
 2. Kiswahili
 3. # 1
 • Kurasa :
 • 1


Hakuna maoni yoyote kwa sasa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni yako!
Guest
Wasilisha Maoni Yako
Sakinisha faili au picha kwenye mjadala huu kwa kubonyeza kitufe cha sakinisha hapa chini. Inapokea gif,jpg,png,jpeg,zip,rar,pdf
• Insert • Futa Sakinisha faili (Lisizidi ukubwa wa: 2 MB
Weka Eneo Ulipo

Kuweka eneo ulilopo wakati wa kutoa maoni yako inawezesha wajumbe kujua mahali ulipo.

Latitude:
Longitude:

Jukwaa la Elimika

Mijadala

Afya
 1. Mijadala 6
 2. MIjadala midogo
Kiswahili
 1. Mijadala 20
 2. MIjadala midogo
Michezo
 1. 1 post
 2. MIjadala midogo
Teknolojia
 1. Mijadala 8
 2. MIjadala midogo
Mchanganyiko
 1. Mijadala 18
 2. MIjadala midogo

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search