"Elimika, Elimisha, Burudisha"

 1. Yose Hoza
 2. Mchanganyiko
 3. Jumatano, 24 Januari 2018
KWA NINI TANZANIA BARA INAITWA TANGANYIKA, NA JINA LAKE LA AWALI KABLA YA KUITWA HIVYO.

Kipindi hicho chini ya utawala wa kijerumani Tanzania ya sasa ilikuwa ikiitwa "Deutsche Ost-Africa".Kuingia kwa waingereza kulipelekea juhudi za kutafuta jina lingine zianze.

Awali mnamo mwaka 1920,majina kadhaa yalipendekezwa yakiwemo "Smutsland","Ebumea","New Maryland","Windsorland" na "Victoria".Hata hivyo majina hayo yote yalikataliwa na serikali ya uingereza kutokana na sababu mbalimbali.

Baadaye serikali ya uingereza ilielekeza yapendekezwe majina ya kienyeji na kwa mwanya huo ndipo yakajitokeza mapendekezo ya majina ambayo ni "Kilimanjaro" na "Tabora"ambayo yalifikiriwa lakini hayakukubalika.

Hatimaye jina "Tanganyika protectorate"lilipendekezwa na msaidizi wa Waziri Wa Makoloni na likakubaliwa na serikali.

Ifahamike kwamba kabla ya ujio wa wageni kutoka ulaya,wenyeji katika maeneo ya magharibi mwa nchi waliliita ziwa kubwa lilopo eneo hilo "ziwa Tanganyika".

Inaelekea kuwa hiyo ndiyo sababu kuu ya kuwafanya maofisa wa kiingereza kulikubali jina la Tanganyika kwa sababu lilikidhi matakwa ya Sera kwa kuwa lilitokana na majina ya kienyeji.

Hatimaye baadae neno "protectoratehi"liliondolewa kutoka jina rasmi la "Tanganyika protectorate" na badala yake likawekwa neno "territory".Kwa hiyo kuanzia mwaka 1920 hadi Uhuru nchi ilijulikana kama "Tanganyika Territory".

Wakati wa kuupigania Uhuru neno territory liliondolewa na Kubaki
"TANGANYIKA".[attachment]FB_IMG_1516773057272.jpg
Attachments (1)
Maoni
Hakuna maoni kwa sasa.


Hakuna maoni yoyote kwa sasa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni yako!
Guest
Wasilisha Maoni Yako
Sakinisha faili au picha kwenye mjadala huu kwa kubonyeza kitufe cha sakinisha hapa chini. Inapokea gif,jpg,png,jpeg,zip,rar,pdf
• Insert • Futa Sakinisha faili (Lisizidi ukubwa wa: 2 MB
Weka Eneo Ulipo

Kuweka eneo ulilopo wakati wa kutoa maoni yako inawezesha wajumbe kujua mahali ulipo.

Latitude:
Longitude:

Jukwaa la Elimika

Mijadala

Afya
 1. Mijadala 6
 2. MIjadala midogo
Kiswahili
 1. Mijadala 20
 2. MIjadala midogo
Michezo
 1. 1 post
 2. MIjadala midogo
Teknolojia
 1. Mijadala 8
 2. MIjadala midogo
Mchanganyiko
 1. Mijadala 18
 2. MIjadala midogo

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search