"Elimika, Elimisha, Burudisha"

Neno Maana
Zoza

Sema kwa kebei, hasira

Udwambidwambi

Yenye kuvutia, mbwembwe, vionjo makini...

Tinginda

Mtu ambaye hababaishwi na jambo lolote.

SHWANGA

Hutumika kuonesha hali ya utulivu, amani na uheri wa afya. Neno 'SHWANGA' hutolewa kama salamu na muitikiaji huitikia vivyo hivyo kwa kulirudia huku akiambatanisha na ishara yoyote ikiwemo kutoa tano (kugonganisha ngumi yake na ile ya anayemsalimia)

PUSU

Ponza, sababisha matatizo mwenyewe

PASU KWA PASU

Sawasawa, nusu kwa nusu, mgawanyo wa kitu kwa ulingano sawa

PAMOKO

Huelezea jambo linalofanyika kwa pamoja/umoja

NYODO

Yenye ujivuni, kujiona, kupenda sifa (madoido)

NOMA

Huelezea maajabu ya kupitiliza; uzuri usio kifani,... yenye kustaajabisha

NDEZI

Kichwa maji... mtu mwenye uelewa mdogo (mpumbavu)

MWANA

Kwa kawaida huonesha hali ya umilikishaji kwa mtu kuwa na mtoto, lakini kwa maana ya kimtaani humaanisha RAFIKI/MDAU wa karibu

Mtoto

Lina maana ya rafiki wa kike unayemkubali na hivyo unalitumia kumsifia. Mfano, 'Yule mtoto niliyekuona naye jana mkali sana.'

MSHIKAJI

Rafiki/Mdau wa karibu. Mara nyingi neno hili hutumika kuonesha ukaribu kati ya mtu na mtu.

Mia

Mia ni neno la mtaani likiwa na maana mambo yako vizuri au safi. Limechukuliwa kutoka kwenye ukamilifu wa shilingi mia moja, yaani mambo si mabaya

Mawe

Fedha, shekeli, Mf. Juma ana mawe sana kuliko wadau wote wa kitaa

Tafuta Neno

Tafuta maana za maneno kutoka kwenye hii kamusi

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search