"Elimika, Elimisha, Burudisha"

Malezi Bora kwa Mtoto

Na UNICEF Tanzania

ADHABU; Humuumiza mtoto na kumpa madhara ya kimwili. Mara nyingi adhabu hutumika kukidhi mahitaji ya mlezi kupitia mtoto.

Adhabu huleta hasira na chuki ambayo haisaidii kuleta mabadiliko ya tabia kwa mtoto.

Kumuadhibu mtoto kunaweza kumfanya aziache njia  potovu lakini bado haitoi mchango chanya kwa maendeleo yake.

Mtoto hujifunza kwa kuonyeshwa namna ya kuwa na tabia nzuri, kupewa maelezo yaliyo wazi kuhusu kinachotarajiwa kutoka kwao.

Mtoto hujifunza kwa kupendwa na kuthaminiwa, na kusifiwa anapofanya mambo sahihi.

MUHIMU: Kuna hatari kubwa ya kumuumiza mtoto ikiwa mzazi atatumia adhabu ya kumpiga.

Adhabu ya kupiga mtoto: Inaweza kuleta madhara ya kimwili, ulemavu wa kudumu wa mwili na mara kadhaa kifo.

Adhabu ya kupiga mtoto: Kuna hatari kubwa ya kumjengea mtoto matatizo ya kihisia katika maisha yake ya baadae.

JE WAJUA? Watu wengi walioadhibiwa wakiwa watoto hunyanyasa watoto wao na familia zao wanapokuwa watu wazima.

Mtoto hujifunza kwa mifano; anapoona watu wanaonesha hasira nakudhibiti wengine kwa kupiga, hujifunza kufanya vivyo hivyo.

Wazazi mara nyingi huwapiga watoto wao wanaposhindwa kujitawala au wanapopatwa na hasira na siyo kwa sababu wamechagua kupiga kama njia ya kuwashawishi watoto wao kuwa na tabia inayofaa.

KUMBUKA: Kadri adhabu inapokuwa kali zaidi ndivyo inavyopelekea mtoto kuwa na matatizo. Kama  kutojithamini, kuwa mhalifu, kupata magonjwa ya akii na kuwa na tabia ya ukatili.

Wazazi na walezi wanaweza kutafakari juu ya maswali yafuatayo kuhusu njia za nidhamu wanazotumika.

Je kusudio la adhabu ni kumuelimisha mtoto au namna ya kutoa hasira ya mzazi mhusika? 


Je mtoto ana uwezo wa kuelewa uhusiano kati ya tabia yake na adhabu inayotolewa?

Je adhabu inayotolewa inafaa na iko ndani ya mipaka ya nidhamu inayokubalika?

Je ipo adhabu nyingine ambayo si kali kama hiyo lakini yenye uwezo wa kuleta matokeo yanayotakiwa?

Je adhabu hii ni ya kushusha hadhi ya mtoto, ni ya kikatili na inavuka mipaka ambayo mtoto anaweza kuvumilia?

Kama nguvu inatumika, je itatumika kwa uangalifu ili kuepusha kujeruhi?

Maswali haya yanasaidia kuweka mipaka kati ya nidhamu inayokubalika na unyanyasaji wa kinjinsia.

Basi sasa tuangalie nidhamu

NIDHAMU: Hujumuisha mbinu za kumfundisha mtoto juu ya kujitawala na kuishi katika tabia zinazokubalika katika jamii.

Nidhamu ni sehemu muhimu katika mahusiano ya mtoto na mzazi. 


Ina lengo la kukuza uwezo wa utawala wa ndani wa mtoto unaomsaidia kujenga mahusiano chanya na wenzake na kuishi kiungwana.

Nidhamu ni sehemu muhimu katika mahusiano baina ya mtoto na mzazi

Inahusisha mchakato wa elimu, miongozo na kujifunza namna nzuri ya kuwasaidia watoto kujitawala.

Nidhamu inajidhihirisha katika kuheshimiana na kuaminiana baina ya mtoto na mzazi.

Inajikita katika imani kuwa mtoto atakuwa radhi kubadilika kwasababu ya kuwepo kwa kuheshimiana au uelewa mkubwa zaidi

Ili kuimarisha tabia njema - Ona zaidi matendo mema yanayofanywa na mtoto badala ya yale ambayo huyapendi.

 

Jaribu kutoa maoni juu ya hayo matendo mema na uhakikishe mtoto ametambua kuwa umeyaona na kupendezwa nayo.

Njia hii itamfanya asiwe na tabia mbaya/kufanya makosa ili kuvuta wema na usikivu wako.

Mpe mtoto fursa ya kujifunza stadi mpya, mtie moyo badala ya kumlaumu anapofanya makosa. Hayo ndo malezi bora.

Kumbuka daima kuwa wewe ni mfano wa tabia unayotaka mtoto wako ajifunze.

Kama kuna hali inayokufanya ukasirike sana jaribu kujiondoa kwenye hiyo hali hadi pale utakapokuwa umetulia.

Usimdhalilishe au kumfedhehesha mtoto kwani mambo hayo yanaweza kujenga chuki nakushusha kujithamini kwa mtoto.

Jifunze hatua ya makuzi ya tabia kwa umri wa mtoto wako.

Mara nyingi tuna matarajio ambayo hayana uhalisia kwa watoto na vijana wetu na hatutambui kuwa kila mara hawana uwezo
wa kufanya mambo tunayo kiri.

Mara nyingine tunaelezea tabia zao kama za “kitukutu”au “kikaidi”wakati ni tabia za kawaida katika ukuaji.

Jadili na mkubaliane juu ya kanuni na mipaka, mshirikishe mwanao mambo mbalimbali yaliyo ndani ya uwezo wake.

Mtoto huzingatia kwa umakini zaidi kanuni kama alishiriki katika kuzijadili na kuelewa sababu za uwepo wa kanuni hizo.

Hakikisha mtoto anajua matokeo ya tabia zisizokubalika kabla ya kujiingiza katika tabia hizo.

Kwa namna hiyo watakuwa na chaguzi. Fanya matokeo kuwa ya kawaida na yahusiane na matukio kwa kadri inavyowezekana.

Tunatumai kuwa umepata kitu cha kujifunza kuhusu MALEZI BORA ya mtoto. Shukran za dhati kwa timu nzima ya #ElimikaWikiendi kwa nafasi

0
0
0
s2sdefault

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search