"Elimika, Elimisha, Burudisha"

Manufaa ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa mama, mwana na familia: kiafya, kiuchumi na kijamii.

Na UNICEF Tanzania

Kila mwaka kuanzia tarehe 1-7 Agosti, Tanzania huungana na nchi nyingine kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama Duniani.

Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji yana kuhamasisha, kulinda na kusaidia unyonyeshaji bora wa maziwa ya mama na pia kuweka.

Kauli Mbiu ya mwaka huu wa 2017 inasema “SOTE KWA PAMOJA TUENDELEZE UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA”.

Hii ina maana wadau wanapaswa kuhakikisha kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni endelevu ili kufikia Malengo ya dunia 2030.

Wadau wa unyonyeshaji ni pamoja na watunga sera na miongozo mbalimbali (wanasiasa na wataalam mbalimbali), waajiri , wanafamilia, wenza, bibi, marafiki, viongozi wa jamii, viongozi wa dini na watoa huduma za afya katika ngazi mbalimbali.

Unyonyeshaji wa maziwa ya mama una manufaa kwa mama na familia: kiafya, kiuchumi na kijamii.

Una gharama ndogo ukilinganishwa na ulishaji mtoto maziwa au vyakula vingine.

Unyonyeshaji hujenga mahusiano mazuri kati ya mama na mtoto hivyo kusaidia katika makuzi bora ya mtoto.

Unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni muhimu sana kwa afya na uhai wa mama na mtoto. 

Maziwa ya mama yanaendelea kumpa mtoto asilimia 50 ya nguvu ambayo mtoto huhitaji katika umri wa miezi 6-12.

Na asilimia 35 katika umri wa miezi 12-24 hivyo, maziwa ya mama ni sehemu muhimu ya mlo wa mtoto.

Mtoto anayenyonyeshwa vizuri anapata kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Na hivyo kuwezesha wazazi na familia kutumia muda wa kutosha kushiriki katika shughuli mbalimbali za kuongeza kipato kama kilimo ufugaji au biashara.

Unyonyeshaji wa maziwa ya mama una mchango mkubwa katika kulinda uhai, afya na ustawi wa watoto wachanga/wadogo na mama zao

Mtoto asiponyonyeshwa kwa usahihi kuna uwezekano mkubwa wa kupata utapiamlo.

Mtoto mwenye utapiamlo huugua mara kwa mara, na anakuwa na maendeleo dhaifu ya ukuaji kimwili na kiakili.

Mtoto aliyepata utapiamlo ana uwezekano wa kudumaa na hivyo kuathirika kiakili na kimwili.

 Hii husababisha ugumu wa kufikia elimu ya juu, hiyvo kuwa na mchango mdogo katika kukuza uchumi na hivyo pato duni la taifa.

Maziwa ya mama ni chakula asilia, hutengenezwa wakati wote bila kuleta uchafuzi wowote wa mazingira

Na pia maziwa ya mama hayahitaji makopo ya kuhifadhia.

Viwanda vya kutengenezea maziwa mbadala, kwa upande mwingine, vina mchango katika uchafuzi wa mazingira.

Maziwa ya mama siyo tu salama na bora katika kulinda afya ya mtoto bali pia ni chakula kinachosaidia kulinda mazingira yetu.

Basi unyonyeshaji husaidia kuifanya dunia yetu kuendelea kuwa na mwonekano wa asili.

Vilevile, maziwa ya mama ni ulishaji endelevu kwa watoto wachanga na wadogo.

Ikumbukwe kuwa unyonyeshaji sio suala la wanawake pekee yao bali ni jukumu letu sote.

Mama apatiwe msaada wa kunyonyesha mtoto wake kutoka kwenye familia, mitandao ya jamii, kazini, serikalini na vituo vya afya

0
0
0
s2sdefault

WASILIANA NASI

Elimika, Ghana Avenue, Posta House
SLP: 73622 Dar Es Salaam, Tanzania
Simu: 0764 006 222
Barua Pepe: info@elimika.co.tz

UNGANA NASI

VIGEZO NA MASHARTI

Ni haki yako kuzifanya taarifa zako kuwa za siri, hivyo basi, taarifa zako ni siri yako na hazitasambazwa popote ila zile zilizo upenuni, zitatumika kwaajili ya maendeleo ya jukwaa hili. Soma Zaidi

©2018 Elimika. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imeundwa na SphereCom.

Search